FKF KUSHIRIKIANA CAF NA FIFA

Rais mpya wa fkf Hussein Mohamed amesema kuwa analenga kutumia ofisi yake kuchochea makuzi ya soka katika ukanda huu wa afrika mashariki lakini pia afrika kwa jumla.

Akizungumza hiyo jana katika kikao na viongozi wengine wa michezo jijini Nairobi Hussein anasema analenga kufanya kikao na rais wa soka Afrika CAF Patrice Motsepe pamoja na rais wa FIFA duniani Gianni Infantino kupanga mikakati ya kuboresha soka akisema kuwa kwa sasa mchezo huo unauwezo wa kutumika kama kitega uchumi kikubwa kwa wananchi wa Afrika.

”Tayari nimeongea na rais wa CAF na Fifa tunapanga kufanya vikao vya kuinua soka la ukanda huu kwa manufaa ya Afrika kwa jumla.” Alisema Mohamed

Vile vile ametuma wito kwa serikali ya Kenya kupitia wizara ya michezo kuchukulia michezo kuwa kitega uchumi badala ya kubezwa kama ilivyokuwa miaka ya awali. Hussein amesistiza kuwa hio ni kati ya njia za kuwakwamua malilioni ya wakenya katika umaskini na kuwapa ajira.