Mmiliki wa klabu ya Young Bulls Johson Mwabati anazidi kukashifiwa kwa hulka yake ya kusababisha fujo katika mechi hasa kipindi ambacho maamuzi yenye utata yamefanywa na refa wa katikati ya uwanja dhidi ya klabu yake.
Kocha wa Congo Boys Kelvin Omondi anadai kuwa hali hiyo inafaa kusitishwa mara moja kwani sio sahihi kwa kiongozi kama huyo kuonyesha tabia kama hizo.
”Tukio la kusababisha sarakasi kama vile halifai kabisa katika soka leta na anafaa adhibitiwe au ajirudi na tabia hiyo aikomeshe, sio ustaarabu” alisema Omondi
Omondi ameyasema hayo baada ya matukio ya fujo za Mwabati katika uwanja wa Alaskan Congo Boys ilipochukua ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Young Bulls iliyokuwa iko nyumbani.
Omondi vilevile anasema msimu huu klabu yake kutoka kule kaunti ya Mombasa imeimarika zaidi baada ya kufanya usajili wa kutosha akiahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa na imani kuwa msimu huu watamaliza katika nafasi nzuri.

