Ipo haja ya viongozi wa fkf katika kaunti ya taita Taveta kushirikiana pamoja na wale waliopoteza katika uchaguzi wa matawi mwezi huu kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya soka la kaunti hiyo.
Ni kauli ya Mohamed Hassan maarufu kama mzazi mzoefu kocha mkuu wa klabu ya Teita Estate ambaye anasistiza kuwa viongozi wa fkf kwa sasa waache siasa na badala yake washirikiane kwa pamoja kubadilisha hali ya mchezo huo mashinani.
Mohamed ameshauri viongozi wa fkf kushirikiana na serikali ya kaunti ya Taita Taveta ili kuboresha miundomsingi muhimu ya kujenga ubora wa soka la vijana mashinani akihoji kuwa kujenga ubora wa soka sio kazi ya shirikihso pekee hivyo kila mtu anahitajika.
Hayo yanajiri huku wikendi hii Teita Estate ikipanda hadi nafasi ya kwanza kwenye ligi ya daraja la pili na alama 15 baada ya mechi sita. Jumamosi klabu hiyo ya mwatate iliipiga Beach Bay bao 1-0 pamoja na kuitandika Inter Dabaso 1-0, mechi zote zikiwa ugenini.

