Maafisa wanaowakilisha Shirikisho la Soka Afrika CAF kwa sasa wapo nchini Kenya kwa ajili ya ukaguzi wao wa pili ili kutathmini utayari wa taifa hili kuandaa mashindano ya CHAN mwaka ujao wa 2025.
Taarifa zasema kuwa ujumbe wa CAF uliwasili jana a, na kuanza ukaguzi wao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).
Kama kitovu cha msingi cha wanaowasili kutoka mataifa ya nje, JKIA ina jukumu muhimu katika kuhakikisha upangaji mzuri wa wachezaji, maafisa na mashabiki.
Kulingana na ratiba iliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), maafisa wa CAF leo watakagua Uwanja wa Nyayo, pamoja na Uwanja wa Police Sacco, na Ulinzi Sports Complex kama viwanja vinavyoweza kufanyia mazoezi.
Kesho, maafisa hao wataelekeza nguvu zao katika Uwanja Mkuu wa Kasarani, Kasarani Annex na Uwanja wa Chuo cha Michezo cha Kenya.
wawakilishi hao watahitimisha ziara yao kwa mkutano wa mapitio ya ziara hiyo na maafisa wa Kenya kabla ya kuondoka Jumamosi.