Bishop Athony Muema ambaye ni mwenyekiti na mdhamini mkubwa wa klabu ya Biringi Sharks inayoshiriki katika ligi ya kaunti ya Kilifi anasema licha ya tukio la dhulma ya baadhi ya wachezaji kufuja pesa za zawadi za mashindano ya Governors Cup msimu uliopita katika kaunti hiyo msimu huu analenga kusajili wachezaji wengine wapya baadala ya kuachana kabisa na kuidhamini klabu hiyo.
Amethibitisha kuwa amewatupa nje wachezaji waliokosa nidhamu ya fedha hizo pamoja na kutouheshimu uongozi wa timu hiyo.
Hata hivyo ameapa kutoruhusu timu yake kujihusisha katika mashindano ya aina yoyote ambayo sio ya ligi ya fkf kwani amejifunza kutokana na mashindano yalopita ambayo anadai kuwa yalimharibia heshima katika kikosi chake.
”Msimu ujao timu yangu itashiriki ligi, nimepanga kuiregesha timu katika ligi na wachezaji wengine kwa sababu sikupenda hilo jina la Biringi Sharks liishe tu hivyo. Wachezaji wangu sitawahi kuwaruhusu wacheze katika mashindano mengine kama si ligi ya FKF” Alisema Muema

