Klabu ya Teita Estate kutoka Mwatate kaunti ya Taita Taveta inazidi kuandikisha matokeo bora msimu huu katika ligi ya daraja la pili kutokana na motisha wachezaji wanaopewa na wadhamini wao.
Kulingana na kocha mkuu wa klabu hiyo Mohamed Hassan ukipenda kocha mzoefu anasema wachezaji wake wote wameajiriwa na kampuni ya makonge jambo ambalo linawafanya kutuliza mawazo na kuzingatia kusakata kabumbu bila shinikizo la changamoto za kiuchumi katika maisha yao binafsi.
Mohamed ametuma wito kwa wawekezaji wengine katika mkoa huu wa pwani kuja mashinani na kuzipa sapoti timu za mkoa huu ili kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo zile za kifedha na usafiri. Amesema kusaidia kulea vipaji vya soka sio kazi ya shirikihso peke yake bali ni jukumu la watu wanaozunguka jamii kwa jumla.
Teita Estate inazidi kuwa na msimu mzuri baada ya kupigwa mechi moja pekee msimu huu na imesajili alama 15 na sasa ndio klabu inayoongoza ligi ya daraja la pili kitaifa.

