YANGA YAIOMBA YOUNG BULLS MCHEZAJI WAO

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga FC Collins Omol anaiomba klabu ya Young BULLS inayoshiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa kumwachilia mchezaji wao Soldeir Kaiungu ajiunge na klabu ya Yanga baadala ya kumwacha nje ilhali hajakuwa akishirikihswa katika mechi ya Young Bulls.

Omol ambaye klabu yake iko daraja la pili anawarai Young BULLS kumwachilia Kaingu japo kwa mkopo aisaidie Yanga kwa sababu wamekuwa wakifanya naye mazoezi kwa majuma mawili sasa baada ya kutoka Young Bulls.

”Tunaiomba klabu ya Young Bulls impe release mchezaji huyu ili sisi tumtumie na wakimhitaji tutawarudishia” Alisema Omol

Omol anasema Yanga itakuwa tayari kumrudisha Solder kwa klabu yake wakati atakapohitajika mwisho wa msimu badala ya kubaki mtaani bila kucheza ikizingatiwa kuwa mchezaji mwenyewe amependelea kucheza Yanga.

Kwa mujibu wa ripoti za mashinani ni kuwa Soldier kaingu ameachana rasmi na klabu ya Young Bulls na tangia msimu uanze hajakuwa akicheza mechi zozote au kujihusisha na klabu hiyo ya Malindi High.