JUNIOR FC IMEJIPANGA KWA MSIMU UJAO

Timu ya Junior Fc kutoka kaunti ya Taita Taveta ambayo ikishiriki ligi ya daraja la pili msimu jana kwa mara ya kwanza inalenga kuendeleza matokeo bora msimu ujao.

Kulingana na kocha mkuu wa kikosi hicho Zablon Mwale ni kuwa wanapanga kuanza msimu kwa kishindo, na sasa wamefanya usajili wa wachezaji takriban saba watakao watumia msimu huo

”Tumeamua msimu ujao tukiwashe kwenye ligi, tumesajili wachezaji saba baada ya majaribio ya wachezaji tuliofanya hivi karibuni” Alisema Mwale

Mwale ameongeza kuwa talanta zipo katika kikosi chake ila tatizo ambalo sasa ni sugu kwao ni ukosefu wa hela, anasema msimu jana mbali na changamoto nyingine hili liliwaathiri sana kama klabu.

”Changamoto zetu kama kawaida imekuwa pesa, i wish tungekuwa na mdhamini lakini pamoja na hiyo uchovu msimu jana ulitulemea.” Aliongeza Mwale

Msimu mpya wa daraja la pili utaanza rasmi  tarehe 2 mwezi November mwaka huu.