TOM ALILA AAHIDI LUINUA SOKA LA MASHINANI

Tom Alila ambaye ni mwaniaji wa Urais wa Fkf anasema analenga kuimarisha soka la mashinani iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Fkf mwaka huu kwenye kura za urais zitakazofanyika mwezi Disemba

Alila amesema ipo haja ya kuimarisha soka la mashinani kwani hilo ndio hujenga soka la kitaifa akitolea mfano Junior starlets ambayo ikishiriki mashindano ya Dunia ya FIFA akitaja kuwa ni timu iliyotokea mashinani.

Alila anasema iwapo hata soka la shule za upili au hata zile za msingi litaboreshwa huenda Kenya ikaimarika kisoka. Anasema hamasisho la soka shuleni pamoja na mafunzo yanaweza kusaidia kuanza kulea vipaji na kuunda timu za wachezaji wachanga mapema kabisa ikizingatiwa kuwa mara nyingi wanafunzi wako shule