TOM LANGO AJIONDOA KWENYE KINYANG’ANYIRO CHA FKF

Mwenyekiti wa Fkf katika tawi la eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi Bwana Tom Lango ametangaza kujiondoa katika kipute hicho kutokana na kuvamiwa pamoja na kutishiwa maisha yake.

Kulingana na Tom ambaye amethibitisha kwa Tama La Spoti ni kuwa alivamiwa na vijana takriban ishirini wakiwa wamenifunga vitambaa na kuficha nyuso zao wakiwa na silaha na kumtishia akiwa na familia yake katika mtaa wa Kisumu Ndogo katika mji wa Malindi kaunti ya Kilifi.

Ujumbe wa watu hao ambao bado hawajajulikana Kulingana na Tom wanasema kuwa kiti ya uenyekiti wa soka la kaunti ya Kilifi ni sharti kimikikiwe na mmijikenda, Lango anasema kutokana na majadiliano ya masaa mengi na familia yake ameamua kujiondoa.

Tom Lango anasema ameripoti kisa hicho kwa Maafisa wa polisi na kwa sasa anaendeleza likizo yake kipindi hiki ambacho ligi zimesimama.

Uchaguzi wa Fkf unatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi ujao huku ule wa urais ukifanyika tarehe 7 mwezi Disemba