Timu ya taifa ya Junior Starlets ambayo iko Dominican Republic kwa ajili ya mashindano ya kombe la dunia ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 imeipiga Dominican Republic kichapo cha mabao 3-1 katika mechi ambayo ni ya miwsho ya kirafiki kabla ya mashindano rasmikuanza tarehe 16 mwezi huu.
Kenya ilianza kwa kuruhusu bao lakini ikakomboa kupitia Valare Nekesa, Marion Serenge akaifunia Kenya bao la pili na kisha Lindey Atieno akafunga bao la tatu na kuipa Kenya ushindi huo.
Kikosi hicho cha kocha Midred Cheche kimejitayarisha vilivyo kwa mashindano ya kombe la dunia ambayo ni historia kwa taifa hili kwani ndio timu ya kwanza katika soka la Kenya kuwahi kushiriki katika mashindano haya ya FIFA.
Mechi ya kwanza kwa Junior Starlets ni tarehe 18 mwezi huu ambapo watakuwa wanavaana na timu ya taifa ya Uingereza

