Kipa nambari moja wa Liverpool Allison Becker atakosa mechi sita za klabu hiyo baada ya kupata jeraha la paja wikendi ilopita
Alison alitumia katika mechi ambayo Liverpool ilishinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Crystal Palace na kutoka kunao dakika ya 79
Taarifa zasema kuwa atarejea baada ya mapumziko ya kimataifa mwezi November mwaka huu 2024.
Kufikia sasa Becker amekuwa na kiwango bora msimu huu akifungwa mabao mawili pekee katika mechi ambazo ameichezea Liverpool chini ya kocha Arne Slot.
Raia huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 32 atarejea katika mechi dhidi ya Southampton tarehe 24 mwezi November. Caoimhin Kelleher ambaye alikosekana katika mechi dhidi ya Palace Jumamosi kutokana na ugonjwa atachukua viatu vya Ali kuelekea mechi zijazo.

