BARRY OTIENO AJIUZULU

Katibu wa soka la Kenya Barry Otieno amejiuzulu kutoka wadhifa huo hii leo baada ya kuhudumu kwa miaka mitano katika ofisi ya afisa mkuu mtendaji

Kufuatia tukio hilo Fkf imetangaza Patrick Korir kama mtendaji mkuu wa muda kuchukua nafasi ya Barry Otieno.

Kabla ya kuteuliwa katika FKF, Korir alihudumu katika wadhifa sawa na Klabu ya Ligi Kuu ya Kenya, Nairobi City Stars.

Korir ni msimamizi mwenye uzoefu wa juu, na historia ya muda mrefu katika soka.Korir atashikilia jukumu hilo kwa muda mfupi na mabadiliko haya yanajiri kipindi ambacho soka la kenya linatarajia uchaguzi mkuu kufanika tarehe saba mwezi disemba mwaka huu.