KAMATI YA UCHAGUZI YATANGAZA SIKU YA MWISHO YA KUWASILISHA LALAMA

Shirikisho la soka Fkf limetangazia vilabu vya mashinani kuwa leo ndio siku ya mwisho kuwasilisha lalama zao kuhusu Orodha ya mwakikishi atakayepiga kura za Fkf.

Kulingana na waraka unaosambaa mitandaoni nikuwa Wadau wa vilabu wanaweza kutuma lalama za yupi anafaa kupiga kura, klabu fulani ambayo haikuorodheswa iwekwe pamoja na kuondoa klabu fulani ambayo haikufaa kupiga kura miongoni mwa masuala mengine.

Lalama hizo zinatumwa kwa Hesbone Owila ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa Fkf nchini Kenya.

Uchaguzi mkuu umeratibiwa kufanyika mwaka huu kabla ya kutamatika kwa mwezi Disemba 2024.