NITAONDOA ADA YA USHIRIKI – TOM LANGO

Mgombea kiti cha uenyekiti wa Fkf kaunti ya Kilifi Tom Lango katika malengo yake iwapo atashinda kura za uchaguzi mkuu mwaka huu analenga kuondoa ada ya ushiriki wa mashindano ya mini ligi ya Fkf ya kaunti.

Amesema iwapo Fkf itapata kufadhili kutoka kwa serikali ya kaunti huenda pia ada ya kushiriki ligi na kujiandikisha akaiondoa kabisa ili vilabu vishirki ligi bila vikwazo vya gharama ya kushiriki mechi za ligi hiyo.

Lango amesema analenga kuhakikisha wachezaji na vilabu bora vinazawidiwa na Fkf tofauti na uongozi wa sasa. Mchezaji bora pamoja na kipa bora wote watapata zawadi.

Tom Lango  anasema uongozi wa sasa katika kaunti ya Kilifi umefeli timu za mashinani.

Kulingana na Lango ni kuwa Dickson Angore ambaye ni Mwenyekiti wa shirikisho katika kaunti ameongoza shirikisho ambalo limefeli katika mambo mengi ikiwemo kuwasilisha msimamo wa ligi kwa wakati, usuluhishwaji wa kesi kwa wakati miongoni mwa mambo mengine ambayo Lango anahisi timu zimekosa kufaidika na uongozi wa sasa.