GRIEZEMANN ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA

Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann ametangaza kustafu soka la kimataifa hii leo.

Griezmann ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2018 ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa X zamani ukijulikana kama Twitter.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Atletico Madrid ameichezea timu yake ya taifa mechi 137 akishindwa tu na Hugo Lloris ambaye katika kikosi cha hivi punde amecheza mechi nyingi, zaidi kabla ya kustafu, Lloris alicheza mechi 145 za timu ya taifa

Katika mechi 137 Griezmann alifunga mabao 44