Klabu ya shabana Fc imepewa adhabu ya kucheza mechi tano za ligi bila mashabiki uwanjani baada ya tukio la Vurugu wikendi ilopita.
Taarifa ni kuwa shabana walisababisha Vurugu katika uwanja wa Ulinzi Complex na kudburu Maafisa waliokuwa katika mechi hiyo.
Kulingana na adhabu shabana watagharamia matibabu ya Maafisa hao pamoja na kukarabati uharibifu wowote katika uwanja wa Ulinzi complex
Madai ya shabana kuwa refa wa mechi hakufuata sheria na kulikuwa na maonevu, lalama zao zimetupiliwa mbali baada ya ripoti ya match commissioner kuthibitisha kuwa sheria zote zilifuatwa kwenye mechi hiyo dhidi ya Ulinzi stars

