Mgombea wa kiti ya uenyekiti cha Fkf kaunti ya Kilifi Tom Lango anadai kuwa ligi za Fkf katika daraja la pili pamoja na ligi ya mkoa zinaendeshwa na ushawishi mwingi kutoka Maafisa wa Fkf kutoka kaunti ya Mombasa
Kulingana na Lango ni kuwa uongozi wa sasa wa Fkf katika kaunti ya Kilifi haujakuwa kipaumbele kutetea timu za gatuzi hilo.
Lango ambaye ni Mwenyekiti wa ligi ya eneo bunge la Malindi ameeleza kusikitishwa na jinsi ambavyo timu za kaunti ya Kilifi zinanyanyaswa kama anavyodai.
” Inasikitisha ligi yaendeshwa na ushawishi kutoka Mombasa. Huku kwetu uongozi umenyamaza tukiona timu zetu zinanyanyaswa. mini ligi yenyewe ilifanyika Mombasa na hata timu za Kilifi zilikuwa zinapiagishwa. Inasikitishwa sana.” Lango alisema
Lango amejitosa katika kampeni na analenga kushindana na mwenyekiti wa sasa Dickson Angore katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

