Huku kocha mpya wa Liverpool Arne Slot akilenga kufanya mabadiliko ya kikosi chake cha kwanza hii leo taarifa zasema kuwa huenda akamleta Federico Chiesa kwa mara ya kwanza katikamechi ya kombe la carabao.
Chiesa aliyesajiliwa kutoka Juventus kwa dau lapauni milioni 13 hajashiriki mechi za Liverpool na huenda usiku wa leo akajukumishwa katika mechi ambayo Liverpool ialenga kutetea ubingwa wa kombe la Carabao katika uwanja wa Anfield dhidi ya Westham United.
Mechi hiyo itachezwa saa nne huku Arsenal na Bolton Wanderers wakitifuana mwendo wa saa nne kasorobo.
Mikel Arteta ametangaza kuwa huenda Martin Odegaard akasalia mkekani kwa takriban wiki tatu baada ya jeraha alilopata akijukumikia timu yake ya taifa ya Norway.

