MOTO WA MBAPPE WAPIGWA BREKI NA JERAHA

Klabu ya Real Madrid imetangaza kuwa Klyan Mbappe atakosekana katika mechi za klabu hiyo kwa takriban majuma matatu kutokana na kupata jeraha la misuli ya paja.

Kulingana na ratiba ni kuwa huenda Mbappe raia wa Ufaransa akarejea kutoka majeruhi baada ya mapumziko ya kimataifa na atakuwa amekosa mechi za Atletico Madrid, Lille pamoja na ile ya dhidi ya Villa Real.

Mbappe ameonekana kuwa na fomu nzuri kwani kufikia sasa amefunga katika mechi tano mfululizo akiwa hadi sasa amefikisha jumla ya mabao 5 na assist moja ya Laliga.

Mbappe anazidi kuwaka moto Kwenye ligi kuu ya Uhispania Laliga baada ya usiku wa kuamkia leo kufunga bao tena kwenye ushindi wa 3-2 dhidi ya Depotivo Alaves.

Ushindi wa jana unaifanya Madrid kuja nafasi ya Pili ligini ama moja nyuma ya Barcelona ambao hawajacheza mechi yao na wakiratibiwa kukitifua leo nyumbani kwao dhidi ya Getafe