HARAMBEE STARS YAWASILI NCHINI LICHA YA KUCHELEWA

Timu ya taifa ya Kenya imerejea nchini usiku wa manane leo kutokana na kuchelewa kwa kusafiri wao baada ya kushuhudiwa mgomo katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Harambe stars ilikuwa Africa kusini ambako ilisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Namibia, mechi ambayo ni ya kutafuta tikiti ya kufuzu kwa AFCON 2025

Kenya itakuwa inachuana na Cameroon mwezi October katika mechi ya mwisho ya kundi lao ugenini. Kipa wa taifa hilo ambaye pia ni kipa wa klabu ya Manchester United Adree Onana amekiri kuwa kikosi anachokiogopa zaidi katika kundi lao Kundi J ni Harambee stars ya Engin Firat.

Katika mechi ya kwanza Harambe Stars ilicheza dhidi ya Zimbabwe iliisha sare tasa, mechi ambayo ilichezwa katika taifa la Uganda kutokana na taifa la Kenya kuwa halina viwanja vya kutosha kuandaa mechi za kimataifa.