LANGO ASEMA ATATOA TAMKO LA MWISHO BAADA YA KIKAO CHA BODI YA UCHAGUZI – FKF

Mwenyekiti wa Fkf katika tawi la eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi Tom Lango amesema kwamba atatangaza mwafaka wake kama atatetea kiti hicho katika uchaguzi wa Fkf ujao baada ya taarifa zitakazitokana na kikao cha kamati kuu.

Lango amesema kwa sasa anasubiri mwongozo kutoka bodi ya uchaguzi wa Fkf na kwa sasa lengo lake kubwa ni kuimarisha uendeshwaji wa ligi ya eneo bunge lake.

Lango amethibitisha kuwa ligi ya eneo lake inaufuagiliwaji mkubwa tofauti na ligi nyingi za mashinani akidokeza kuwa mfumo wa kuchapisha matokeo kwa wakati ndio jambo linalowavutia wengi. Amesema kwa sasa kama Fkf wanalenga kusaka mdhamini ili kuboresha hadhi ya dimba hilo.

Wikendi ilopita FKF yake Lango iliandaa mashindano ya Mini League na kutuza mabingwa wa ligi katika hafla ilofanyika kwenye uwanja wa Alaskan