Klabu ya SS Assad imethibitisha kumsaini Feyswal Dzuya kutoka klabu ya GFC ya Gongoni eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Feyswal ambaye ni Mchezaji bora wa pwani katika mashindano ya Soka Super Cup taarifa zasema kuwa alikuwa Kwale hiyo jana kwenye uzinduzi wa jezi na kukubali kusaini na miamba hiyo ya kwale.
Sasa Feyswal ambaye amekuwa akiwindwa Sana na vilabu kadhaa ikiwemo Young Bulls ya malindi ataichezea SS Assad ya kwale inayoshiriki ligi ya kitaifa ya Super League hii ikiwa ndio ligi kubwa ya FKF kwa mzawa huyo wa mjanaheri kuwahi kushiriki.

