James Mboso Baraka mchezaji wa klabu ya Babylon kutoka Gongoni eneo bunge la Magarini anafikiria kurejea katika klabu yake ya zamani Beach Bay.
Kiungo huyo aliyengaa katika mashindano ya hivi punde zaidi ya Dola Super Cup anafikiria kuanza msimu mpya na kocha James mkutano katika ligi ya daraja la pili.
Huku hayo yakijiri Hassan Mwambegu, fowadi anayekipiga katika klabu ya Matano Mane Youth taafifa zasema kuwa anasakwa sana na klabu ya Mombasa Stars.
Mwambegu maarufu kama Lukaku ni Kati ya wachezaji waliongaa sana katika mashindano ya Dola Super Cup pia akifunga bao la kuikomboa kilifi katika mashindano ya kimkoa huko Mombasa wikendi ilopita ambapo Kilifi ili shinda kwa matuta baada ya tisini mechi kuisha ikiwa sare ya bao 1-1

