LUCKY LEWA AWINDWA MOMBASA

Nyota wa klabu ya Mbungoni FC kutoka eneo bunge la rabai Lucky Lewa anavutia vilabu kadhaa vya Mombasa.

Klabu ya Mombasa Stars inayoshiriki ligi ya kitaifa ya NSL ni kati ya vilabu ambavyo vimeonesha nia ya kumsajili Lewa.

Mshambuliaji wa klabu ya Tsunami Fc Mohamed Modizo ameivutia Young Bulls inayoongozwa na Kocha Ali Mwachaunga ambaye analenga kukiimarisha kikosi hicho kuelekea msimu mpya.

Hata hivyo Modizo ameashiria kuwa kwa sasa hayupo tayari kuelekea Malindi High na badala yake kusalia Magarini msimu ujao.

Ikumbukwe kuwa kocha wa sasa Ali Mwachaunga ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja lengo lake ni kuipandisha Young Bulls ligi ya kitaifa ya NSL ndiposa kwa sasa yupo mbioni kunasa wachezaji watakaomsaidia kukamilisha mradi Huo.