KILIFI SOUTH YAFUZU FAINALI ZA DOLA SUPER CUP

Timu ya soka ya kilifi South inayowakilisha kaunti ya Kilifi katika mashindano ya dola super Cup hatua ya mkoa wa pwani yanayoendelea katika kaunti ya Mombasa imetinga fainali ya michuano hiyo.

Kilifi imefuzu baada ya kuipiga Kwale B kichapo cha bao 1-0 katika uwanja wa Mombasa Sports Ground. Bao la pekee na la ushindi katika mechi hiyo limefungwa na Feyswal Dzuya kunako dakika ya 4 ambaye jana pia alifunga bao 2-0 akitokea benchi.

Sasa Kilifi wanasubiri mshindi wa Kesho kati ya Mombasa A dhidi ya Mombasa B.

Mashindano haya yanatamatika rasmi siku ya Jumapili ambapo mshindi wa fainali za pwani atajishindia milioni moja kutoka kwa wadhamini Dola Group.