Ni afueni kwa klabu ya Shabana FC inayoshiriki katika ligi ya fkf premier league hapa nchini Kenya baada ya kufanikiwa kusaidi dili la udhamini na kampuni ya sportpesa.
Shabana Fc ukipenda Tore Bobe imesaini dili la udhamini wa milioni 75 ambao utagawanya katika awamu tatu sawa na milioni 25 kila msimu.
Haya yanajiri baada ya Shabana kupitia changamoto chungu nzima msimu uliopita katika ligi ya fkf.
Klabu hiyo sasa inaendelea kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya ambao unaanza hapo kesho na shabana wameratibiwa kusafiri mpaka Thika ambako watakuwa wanachuana na vijana wa Bidco United.
Mwenyekiti wa klabu ya Shabana FC, Jared Nevaton ameelezea matumaini ya timu hiyo kutamba zaidi kwenye ligi kuu soka nchini FKF msimu ujao licha ya kukumbwa na changamoto si haba msimu jana .
Shabana FC ilikabiliwa na tishio la kushushwa daraja kutoka ligi hiyo kuu huku wakinusurika mwishoni mwa msimu. Mwenyekiti huyo ana imani kuwa masomo waliopata yatasaidia kuimarika msimu huu.

