WADADA WA PWANI WAOMBA SAPOTI MICHEZONI

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali wakiwemo serikali, wafanyibiashara na jamii kwa jumla kuwekeza katika soka la kinadada iwapo wangependa kuona soka hilo likikua na kufaidi wasichana wa mkoa huu wa pwani.

Ni kauli ya Elizabeth Santa naibu mwenyekiti wa Kilifi Women Soccer Forum wakati akizungumza na Lulu FM. Santa ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya MTG amesema kuwa soka la kinadada kwa sasa liko chini sana mashinani kutokana na changamoto nyingi wanazopitia.

Santa amethitisha kuwa pia ipo haja ya kuanzisha na kuwezesha ligi za mashinani katika kaunti ya Kilifi ili kusaidia kuufanya mchezo wa soka wa kinadada kuwa maarufu pamoja na kuwezesha kuvumbua talanta za wachezaji wengi ambao wanaweza kuwa muhimu katika vikosi vya taifa.

Kwa sasa katika kaunti ya kilifi hakuna ligi ya kaunti jambo ambalo linapunguza motisha wa wachezaji wa kike kuja viwanjani.