MURKOMEN ASEMA UONGOZI WA MICHEZO NDIO UMEFELI WAKENYA

Aliyekuwa waziri wa barabara na uchukuzi nchini Kenya Kipchumba Murkomen anasema analenga kuhakikisha kuwa soka la Kenya litapata mwelekeo utakaofurahisha wakenya iwapo atakubaliwa kuwa waziri wa michezo na vijana baada ya kusailiwa bungeni.

Ameyasema hayo wikendi hii katika mahojiano na kamati ya bunge iliyokuwa inaongozwa na spika Moses Wetangula.

Anasema FKF ya sasa inayosimamiwa na rais Nick Mwendwa imefelisha wakenya na hivyo wakati wao umeisha na wanafaa kuondoka katika ofisi hizo.

Murkomen anadai kuwa viongozi wa michezo mbalimbali waliopo nchini Kenya na ambao wamekatalia katika ofisi mbalimbali ndio wanaofelisha michezo kwani wameshindwa kuibadilisha.

Ametolea mfano shirikihso la riadha Kenya pamoja na mashirikihso mengine ambayo yamekaa miaka mingi bila kufanya uchaguzi.