OMANYALA ALEMEWA OLIMPIKI

Mtimakaji mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala ni rasmi sasa ametolewa kwenye mashindano ya olimpiki.

Hii ni baada ya hapo jana kushindwa kufuzu kwa fainali za mashindano alipolemewa kwenye semi fainali kwa muda wa sekunde 10.08 akimaliza katika nafasi ya nane kwenye mbio za mita 100.

Hata hivyo fainali zishafanyika na Noah Lyles mtimkaji kutoka marekani ndiye bingwa wa mashindano hayo kwa muda wa sekunde 9.78. Kishane Thompson wa Jamaica amemaliza katika nafasi ya pili na Fred Kerly raia wa marekani akimaliza katika nafasi ya tatu.

Mary Moraa mwanariadha kutoka Kenya kwenye mbio za mita 800 amefuzu kuingia fainali huku Vivian Chebet akilemewa na kutoka kwenye mbio hizo. Kwenye mbio za mita 1500 ni kuwa brian komen amefuzu kwa fainalisawa na mwezake Timothy Cheruiyot.

Mshindano hayo yanaendelea na yanatarajiwa kuisha rasmi tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu katika taifa hilo la Ufaransa.