BUMBANI STARS NA ZIWANI YOUTH KUTAFUTA TIKITI YA ‘DIV ONE’

Ligi ya daraja la pili kitaifa ilitamatika rasmi wikendi hii na Bumbani Stars ndio mabingwa wa ligi hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora msimu mzima.

Wikendi hii ambayo mechi za mwisho wa ligi zilikuwa zachezwa timu kadhaa zilikosa kuheshimu ratiba kwa kile kinachotajwa kuwa changamoto za usajiri katika mechi za ugenini.

Sango  Sportiff kutoka Tana River walikosa kusafiri kuelekea Tana River kwa mechi dhidi ya Teita Estate na Junior Fc, Yanga kutoka Malindi wakikosa safari yao ya Kwale kuvaana na Vinara wa ligi Bumbani Stars sawia na Kishada kutoka Mombasa waliofeli kucheza na Teita Estate.

Bumbani Stars na Ziwani Youth iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi zitashiriki katika mechi za kuwania tikiti ya kufuzu kwa ligi ya daraja la kwanza kitaifa.