SIKU YA KWANZA YA DOLA SUPER CUP VYUMA VYAKAZA

Kocha wa timu ya Malindi A inayoshiriki katika mashiondano ya Dola Super Cup Hemed Ibrahim amewapongeza vijana wake kwa mchezo wao mzuri baada ya kusajili sare ya bao 1-1 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Kilifi North wikendi ilopita.

Akizungumza na Tama la Spoti Hemed anasema vijana wake walionyesha kiwango bora licha ya kupoteza nafasi nyingi za wazi, hata hivyo anasema katika mechi ya marudiano Malindi A itasajili ushindi wakiwa nyumbani.

Omar Nasir maarufu kama Simba ndiye aliyeifungia bao la kukomboa Malindi A na anasema mchezo wake wa hivi punde umekuwa chini kutokana na jeraha, hata hivo amemshukuru kocha wake kwa kumpa nafasi.

Ali kitsao ambaye ni mchezaji wa Tezo Stars aliyewakilisha timu ya Kilifi North kwenye Dola Super Cup na kuchaguliwa mchezaji bora wa mechi ya ufunguzi amepuzia kauli ya Malindi A anasema wataipiga timu hiyo ugenini.