USIMAMIZI WA YOUNG BULLS YAZUNGUMZIA MSIMU MPYA WA 2024/2025

Usimamizi wa vilabu vya Young Bulls na YoUNG Bulls Starlets umetangaza kuwa unalenga kusimamisha klabu ya wavulana ya Young Bulls kwanza kuwa imara kabla ya kuzamia kuileta klabu ya Young Bulls starlets katika ligi ya fkf msimu ujao.

Kulingana na Shahib Shahib ambaye ni meneja wa klabu ya Young Bulls ni kuwa klabu hiyo ilikuwa na maazimio ya kusajili klabu ya kinadada kwenye ligi za fkf lakini wanasema wanalenga kuchukua muda zaidi kabla ya kuileta klabu hiyo, na kutumia fursa hii kuzidi kuiimarisha ile ya wavulana.

Tofauti na madai ya kuwa klabu hiyo huenda ingelemewa na masuala ya kifedha Shahib amethibitisha kuwa kwa sasa kuna uhaba wa viongozi akidokeza kuwa wale viongozi wanaosimamia klabu ya wavulana ndio wale wale wanaosimamia ile ya wasichana jambo ambalo anasema litalemaza huduma zao.