DR AGGREY KUIWAKILISHA PWANI KWENYE MICHEZO KITAIFA

Kamati ya maamuzi ya michezo ya shule za upili katika mkoa wa Pwani imeirudishia Dr Agrey nafasi yao ya kuiwakilisha pwani kwenye michezo ya shule za upili baada ya taarifa za awali kuwa nafasi hiyo imepewa shule ya Upili ya Tononoka.

Kulingana na taarifa ni kuwa awali Tononoka walikuwa wameshapewa nafasi hiyo na wanaanza Matayarisho lakini maamuzi yakabadilishwa chini ya masaa 24.

Dr Agrey ilikuwa imepokonywa nafasi hiyo na kamati ya michezo ya mkoa kwa kile kinachotajwa kuwa shule hiyo kutoka Taita Taveta ilifoji wachezaji. Hata hivyo kamati ilipofanya tathmini iliafikia kuirudisha Dr Agrey katika nafasi hiyo na sasa vijana hao wa milimani watasafiri kuelekea kaunti ya Kisii kwa Mashindano ya shule za upili kitaifa.

Dr Agrey waliipiga Tononoka kichapo cha bao 1-0 katika fainali ya mkoa katika kaunti ya Tana River majuma kadhaa yalopita na kujipatia nafasi hiyo.