TUZO ZA FKF KUFANYIKA MWISHONI MWA WIKI HII

Shirikihso la soka nchini fkf linalenga kuandaa hafla ya kutuza wachezaji bora wa msimu uliotamatika wa 2023/2024 siku ya ijumaa wiki hii.

Tuzo hizo zitafanyika jijini  Nairobi katika ukumbi wa hoteli ya  Safari Park  kuwatuza wote waliofanya vyema katika vitengo tofauti katika ligi kuu ya wavulana lakini pia ile ya kinadada.

Kulingana na taarifa ni kuwa kuna tuzo la mchezaji bora wa mwaka, mshindi wa kiatu cha dhahabu, mshindi wa glavu ya dhahabu,  refa bora mwaka huu, kocha bora, meneja bora wa mitandao ya kijamii bora pamoja na tuzo ya rais.

Hayo yanajiri huku vilabu vikiwa vinajitayarisha kwa msimu mpya wa 2024/2025 ambapo kwa sasausajili wa wachezaji lakini pia makocha katika vilabu mbalimbali unaendelea.

Klabu ya sofapaka imethibitisha kumsajili kocha wa zamani wa klabu ya Tusker Fc Robert Matano ambaye aliachana na klabu hiyo mkataba wake ulipokamilika mwezi Juni.

Robert Matano mshindi wa ligikuu ya FKF mara tano ambaye pia anaongoza katika wakufunzi ambao wameshinda kombe hilo mara nyinygi anasema analenga kuisaidia Sofapaka kurudia hadhi yake tofauti na miaka ya nyuma ambapo imeyumba kwa muda.

Matano pia anasema analenga kuisaidia klabu hiyo kutafuta wachezaji wapya ili kuifnya kuwa bora kuelekea msimu ujao