Klabu pekee inayoshiriki katika ligi ya fkf daraja la kwanza kitaifa kutoka kaunti ya Kilifi Young Bulls imetangaza kuwa inalenga kuandaa majaribio mashinani katika njia moja ya kutafutawachezaji wapya katika kikosi chao wakitumia vijana wa kaunti hii.
Kulingana na meneja wa timu hiyo Shahib Shahib ambaye amezungumza na Tama La Spoti kupitia njia ya simu mchana wa leo ni kuwa majaribio hayo yanalenga kuwapatia wachezaji wa kaunti hiyo wenye talanta nan matamanio ya kuichezea Young Bulls nafasi katika kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2024/2025.
Shahib amethibitishia Tama La Spoti kuwa klabu hiyo ilitambua baadhi ya wachezaji ambayo imelenga kuwasajili lakini zoezi hilo litafanyika baada ya majaribio na muonekano wa kikosi kabla msimu kuanza ndiposa watazamia kufanya usajili ili kuboresha kikosi na kuziba mapengo ambayo yatajitokeza.
Young Bulls ambayo inashiriki msimu wake wa tatu katika ligi ya daraja la kwanza imesalia peke yake daraja la kwanza la fkf baada ya klabu ya Malindi United inayomilikiwa na mwakilishi wadi mjini Malindi Rashid Odhiambo kuhuka daraja kutokana na msururu wa matokeo mabaya msimu uliopita.

