WANAMICHEZO WAKASHIFU UTEUZI WA MURKOMEN

Rais William Samoei Ruto ametangaza mapendekezo mapya ya baraza lake la mawaziri mchana wa leo na kati waliotajwa ni aluiyekuwa waziri wa barabara na uchukuzi Kipchumba Murkomen kuwa kwenye wizara ya sana, vijana na michezo akichukua mikoba kutoka kwa Ababu Namwamba aliyefutwa kazi siku chache zilizopita.

Ruto huku akiashiria kuwa mapendekezo hayo mapya yakipelekwa bungeni kwa kupigwa musana uteuzi wa Murkomen umepingwa vikali na baadhi ya wananchi ambao Tama La Spoti limezungumza nao alasiri ya leo.

Wengi wao wanasema Murkomen hakufaa kabisa kuwa kwenye wizara hiyo na kwamba Rais amefeli kwenye kupendekeza uteuzi wake.

Murkomen akiwa kwenye wizara ya Uchukuzi na barabara wananchi kadhaa wamesema kwamba hajakuwa na mafanikio yoyote na alikuwa kati ya mawaziri ambao hawakufaa kabisa kutajwa kwenye nafasi yoyote.