Mwanariadha mwenye kasi zaidi barani Afrika kwa rekodi ya sekunde 9.77 Ferdinanrnd Omanyala anasema ana matumaini makubwa na mashindano ya Olimpiki ya paris Ufaransa katika azma yake ya kuiwakilisha Kenya vyema.
Omanyala anasema hana mashaka na kuwa ataandikisha matokeo bora na hii ni baada ya kupata mapumziko ya kutosha baada ya kuacha kushiriki mashindano mawili ya Diamond League ili apate muda wa kutosha kujiandaa.
Kwa sasa Omanyala yupo Miramas katika kambi yake ya mazoezi ambako pia ndio makazi ya muda huu wa mashindano kwa wanariadha wengi waliosafiri kwa jili ya olimpiki.
Omanyala atakuwepo kwenye mashindano muda mchache baada ya sherehe ya ufunguzi itakayofanyika tarehe 26 mwezi Julai.

