Wito umetolewa kwa wachezaji wa soka katika kaunti ya Kilifi kujitokeza kwa wingi na kuonyesha vipaji vyao katika mashindano ya Dola Super Cup yatakayofanyika kuanzia wikendi ijayo.
Kulingana na Suleiman Saddam ambaye ni meneja wa mauzo katika kampuni ya Dola ambayo ndio mdhamini mkubwa wa mashindano haya ni kuwa vipaji vitaangaziwa kwa ukubwa ili kuonyesha ulimwengu talanta za vijana wa mashinani.
Pia Saddam ameonyesha umuhimu wa mashindano ya Dola Super Cup kuwa yanalenga kuleta jamii pamoja huku akirai mashabiki kujitokeza ili kushabikia timu zao.
Mashindano hayo yanaaza rasmi kuanzia tarehe 27 mwezi Julai na kuendelea hadi tarehe 11 mwezi agosti mwaka 2024 ambako mshindi katika fainali atazawadiwa shilingi laki moja 100k huku akielekea katika mashindano ya mkoa wa Pwani yatakayofanyika katika kaunti ya Mombasa, mshindi wa fainali za mkoa atajisindia milioni moja.

