UHAMISHO ULAYA; JAMES RODRUGUEZ, RABIOT, MASON MOUNT

Mchezaji wa timu ya taifa ya Colombia James Rodriguez aliyeshinda tuzo la mchezaji bora katika mashindano ya Copa America 2024 ametangaza kutamatisha mkataba wake ni klabu yake ya sasa Sao Paulo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 sasa ni mchezaji huru kwa klabu yoyote inayohitaji huduma zake.

Rodriguez katika mashindano ya Copa Amerika alifunga bao moja na kutoa assists sita zilizozaa mabao kwenye mechi sita alizoshiriki.

Wakati hayo yakijiri klabu ya Manchester United iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 25, msimu huu wa joto. Hii ni baada ya tetesi za muda kuwa klabu hiyo ya Old Trafford inalenga kuachilia baadhi ya wachezaji. Mount tangia kusajiliwa na Man U amekuwa muda mrefu nje kutokana na majeruhi ya muda.

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, anakaribia kusaini Manchester United baada ya kuondoka Juventus mwishoni mwa kandarasi yake. Hata hivyo mshindi huyo wa kombe la dunia na Ufaransa amekubwa na majeruhi jambo ambalo huenda likatatiza mtazamo wa United kwenye kumsajili kiungo huyo.