SAPOTI YAIPA MAFANIKIO KOMBANI GIRLS

Kocha wa soka katika shule ya upili ya Kombani Girls kutoka kaunti ya Kwale Mukasa Amboko anasema shule yake muhula huu imeweza kutetea ubingwa wa mashindano ya shule za upili hatua ya mkoa kwa wasichana kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na shule hiyo.

Anasema kombani girls imeweka hela za kutosha kuajiri makocha wazoefu wenye vyeti vya CAF jambo ambalo limewasaidia kuandikisha matokeo bora.

Katika mkoa wa pwani Kombani Girls ndio walishinda ubingwa kwenye soka la kinadada na hii ni mara yao ya pili mfululizo kufanya hivyo.

Amboko amesema kwamba muhula huu kombani Girls inalenga kwenda kwenye fainali za kitaifa na kushinda ubingwa baada ya msimu uliopita kutoandikisha matokeo mazuri kwenye kipute hicho.

Mashindano ya shule za upili muhula huu yatafanyika katika kaunti ya Kisii na Amboko anasema mwaka huu watabeba ubingwa na kuelekea katika fainali za Afrika mashariki.