Winga wa timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria ni rasmi sasa amestafu soka la kimataifa baada ya kushiriki mechi yake ya mwisho ya Copa America asubuhi ya leo.
Di Maria ametaja kuwa fainali dhidi ya Colombia ambayo Argentina imeshinda ubingwa wa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo ndio mechi yake ya mwisho kama mchezaji wa kikosi cha taifa kinachoongozwa na Lionel Scaloni.
Di Maria kwa sasa ngazi za klabu atakuwa anaungana na Lionel Messi katika klabu ya Inter Miami huko Marekani baada ya uhamisho wake kutoka klabu ya Benfica kufanikiwa.
Di Maria amejishindia mataji mengi katika ngazi ya kitaifa akiwa kati ya kikosi kilichoshinda Copa America makala yalopita na ya mwaka huu, kombe la fainalisimma pamoja na kombe la dunia 2022 Qatar

