SACRED HEART MOMBASA WASHIRIKI HAFLA YA READ ALOUD

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Sacred Heart Comprehensive School Mombasa wakishiriki katika hafla ya kusoma kitabu kwa sauti maarufu kama Read Aloud kwenye maadhimisho ya siku ya kitaifa ya kusoma vitabu nchini Kenya.

Mpango wa Read Aloud unaendeshwa na shirika la Start A Library Trust chini ya kampunzi ya uchapishaji vitabu ya Story Moja, ambapo shule 14 kutoka maeneo mbalimbali nchini yameongoza halfa hii.

Shirika la Start A Library Trust linalenga kuwashirikisha wanafunzi 3,000 na mabalozi wa kusoma vitabu 6,000 kote nchini huku wakilenga kuvunja rekodi ya dunia ya kusoma kitabu kimoja kwa sauti ambayo kwa sasa inashikiliwa na taifa la Marekani.

Siku ya kitaifa ya kusoma vitabu Kenya maarufu kama Kenya National Reading Day iliidhinishwa rasmi mwaka jana na rais William Ruto kupitia wizara ya Sanaa na Michezo ambapo aliteua tarehe 12 ya kila mwezi Julai kama siku rasmi ya maadhimisho hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *