YOUNG BULLS STARLETS KUINGIA LIGI MSIMU UJAO

Mshauri wa benchi la kiufundi la klabu ya Young Bulls ya kinadada Rishad Shedu  anasema kwamba huenda klabu hiyo ikajisajili katika ligi ya fkf msimu ujao 2024/2025 na kuanza kushiriki ligi za FKF.

Amethibitisha kuwa msimu uliopita klabu hiyo ilishindwa kujisajili katika ligi kutokana na kuchelewa lakini sasa kila kitu kiko tayari na hakuna mashaka kuwa msimu ujao itakuwa kwenye ligi.

Anasema kwa sasa klabu hiyo iko na wachezaji wa kutosha huku ikizidi kuvutia wachezaji wengine kujiunga na klabu hiyo ya kinadada kutoka Malindi kaunti ya Kilifi.

Shedu anasema ipo haja ya vilabu vya wasichana hao pia kupewa sapoti ya kutosha angalau kujiimarisha kwenye ligi na kutimiza ndoto zao za kushiriki ligi ya FKF kitaifa.