Timu ya taifa ya Uhispania imejikatia tikiti ya kufuzu kuingia fainali ya mashindano ya Euro usiku wa kuamkia leo baada ya kuipiga ufaransa kichapo cha mabao 2-1.
Katika mechi hiyo Lamine Yamal kinda mwenye umri wa miaka 16 anayechezea Barcelona aliingia katika historia ya mashindano hayo kwa kuwa mchezaji mchango zaidi kuwahi kufunga bao kwenye Euro.
Bao la pili kwa uhispania limefunga na Dani Olmo huku bao la kufutia machozi kwa Ufaransa likifungwa na Kolo Muani ambaye anachezea klabu ya PSG.
Sasa timu ya taifa ya Uhispania inayoongozwa na Luis Dela Fuente inasubiri kujua mpinzani wao hii leo kwenye semi fainali ya pili itakayokutanisha Uholanzi na timu ya taifa ya Uingereza, fainali ya mashidnano haya itachezwa wikendi ijayo siku ya Jumapili.
Katika mashindano ya Copa America ni kuwa Lionel Messi ameisaidia timu yake ya taifa ya Argentina kutinga fainali ya mashindano hayo baada ya Argentina ambao ni mabingwa watetezi kuichapa Canada mabao 2-0.
Lionel Messi amefunga bao lake la 109 kwa timu yake ya taifa kupitia assist ya Enzo Fernandez huku bao la kwanza likifungwa na Julian Alvarez kinda anayechezea klabu ya Manchester City.
Argentina sasa wanasubiria mpinzani wao wa fainali katika mechi ya usiku wa leo inayokutanisha Uruguay na Colombia mechi ambayo itachezwa saa tisa za asubui ya kesho.

