Mashindano ya shule za upili katika hatua ya mkoa wa pwani yanatarajiwa kuaanza rasmi kesho katika kaunti ya Tana River kwenye shule ya msingi ya Hola na wala sio Oda kama ilivyokuwa kwenye taarifa ya awali.
Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo ni kuwa takriban zaidi ya wanafunzi 1500 wanatarajiwa kuwasili katika kaunti hiyo tayari kwa mashindano.
Mashindano hayo ya siku tatu kwenye muhula huu wa pili yanahusisha michezo ya mpirawa pete, raga ya wanaume na wanadada, soka la wanaume na kinadada. Mpira wa wavu miongoni mwa michezo mingine.
Taarifa zinasema kwamba usalama umeimarishwa hasa katika eneo la Hola ili kuona kwamba wanafunzi wanashiriki mashindano hayo bila taharuki ya utovu wa usalama.