Klabu ya Bumbani Stars kutoka kaunti ya kwale imeanza kufanikiwa katika lengo lake la kufanya vipaji vya wachezaji katika eneo la lungalunga kaunti ya kwale kuonekana kitaifa.
Hiyo ni kulingana na kocha mkuu wa klabu hiyo mwaduka bakari ambaye amesema kuwa mbali na azma ya kupanda madsraja hadi ligi kuu nchini lengo linasalia kuuza wachezaji na kuchipuza wapya ili kuinua michezo ya wachezaji mashinani mwa kaunti nzima ya kwale.
Mwaduka ametaja kuwa wamekuwa wakipata misaada kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo jamo ambalo limewasaidia pakubwa kwenye kuendesha ligi yao hasa kwenye usafiri.
Kwa sasa Bumbani wanaongoza ligi ya daraja la pili kitaifa na matumaini yote sasa yapo kupanda daraja msimu ujao. Klabu hiyo kwa sasa imesalia na mechi tatu pekee zote zikiwa za nyumbani Kikoneni, eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale

