ABABU NAMWAMBA ASHAWISHIWA KUWA NA UWAZI NA OLIMPIKI

Wito umetolewa kwa wizara ya michezo kuweka wazi  orodha ya wachezaji na wadau wote watakao kuwa safarini kuelekea Paris  Ufaransa mwezi huu ambako mashindano ya Olimpiki yatakuwa yanafanyika.

Wito huo umetolewa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya raga ya Kenya Dennis Ombachi ambaye pia ni mkereketwa wa masuala ya michezo humu nchini. Ombachi maarufu kama Roaming Chef kupitia mtandao wake wa X anasema ipo haja ya wizara ya michezo kuweka mambo wazi kwa faida ya wananchi wote wanariadha wakijitayarisha kwa mashindano hayo yatakayoanza rasmi tarehe 26 mwezi huu.

Kufuatia kauli hiyo waziri wa michezo hapa nchini Ababu Namwamba amesema analenga kuachia orodha hiyo kwa wakenya wote akisema wizara hiyo itatafuta muda na sehemu ya kutoa tangazo hilo.

Haya yanajiri baada ya matukio ya awali ambapo katika mashindano makubwa wizara ya michezo na kamati ya olimpiki nchini kumeshuhudiwa ubadhirifu wa feha na kukiukwa kwa utaratibu kwa mfano Olimpiki za Rio 2006 ambako kulikuwa na madai ya fedha kufujwa