Kocha mkuu wa timu ya raga ya shule ya upili ya Marafa Erick Atitwa anasema mabadiliko ya mashindano kutoka raga za wachezaji 15 kila upande hadi 7 kila upande ndio jambo ambalo liliifanya timu yake kulemewa katika mashindano hayo muhula huu.
Marafa Boys ambao walishinda ubingwa wa mkoa wa pwani muhula uliopita na kushiriki mashindano ya kitaifa Machacos anasema walishindwa kustahili ushindani wa mashindano hayo muhula huu na kutolewa katika hatua ya semi fainali katika mashindano ya shule za upili za kaunti ya Kilifi wikendi ilopita.
Atitwa anasema ipo haja ya viongozi wa kaunti za pwani kwa ushirikiano na shule za upili kuja pamoja na kusaidia makuzi ya mchezo huo. Anasema uwekezaji unaofanywa na kaunti nyingi za bara kwenye raga unasaidia kuinua viwango vya mchezo huo katika maeneo hayo tofauti na Pwani ambako raga inapitia changamoto kubwa ya kukosa misaada hasa kifedha.
Mashindano ya shule za upili yatakuwa yanaendelea wiki hii katika hatua ya mkoa wa pwani na yanafanyika Tana River katika shule ya upili ya Oda.

