BANDARI YAIDHAMINI LIGI KWALE

Halmashauri ya Bandari za Kenya KPA imepiga jeki ligi ya Shirikisho la Soka nchini FKF tawi la Kaunti ya Kwale kwa kudhamini ligi ya Kaunti hiyo kwa misimu miwili 2023/2024 na 2024/2025 kwa kitita cha Shilingi milioni 18.

Akizindua udhamini huo kwenye kikao na viongozi 32 wa  vilabu vitakavyoshiriki ligi hiyo ambayo sasa inajulikana kama KPA-KWALE COUNTY LEAGUE,Mwenyekiti wa tawi hilo Hamisi Mwakoja alisema anaimani utazipunguzia timu shiriki gharama mbalimbali zikiwemo ununuzi wa vifaa na usafiri.

Mwakoja alisema udhamini huo pia utasimamia tuzo mbalimbali za washindi na kuongeza kuwa mfomu bora na uwazi katika utendakazi wao  ndio umesaidia kupata udhamini huo. Amewahimiza mashabiki kuzingatia nidhamu kama wangetaka wadhamini zaidi wajitokeze kwa ligi hiyo.